RIPOTI YA 58 NA 59 YA SHUGHULI YA TUME YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU

No : 58-59
Type :
Activity Reports
Language :
Kiswahili
Publisher :
ACHPR

I. MUHTASARI

1. Ripoti zilizounganishwa, ya 58 na ya 59 za Shughuli za Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu (Tume au ACHPR) zinawasilishwa kwa Wakuu wa Nchi na Serikali kwa mujibu wa Ibara ya 54 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu (Mkataba wa Afrika) na zinahusisha kipindi cha kuanzia tarehe 6 Novemba 2024 hadi 30 Oktoba 2025.

2. Shughuli zilizowasilishwa katika Ripoti hii ambazo Tume ilifanya katika kipindi cha mapitio zimelenga kufikia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpago Mkakati wa Tume wa 2021-2025. Kwa hiyo, mikutano ya kisheria ya Tume ililenga hasa kuimarisha mamlaka ya ulinzi kwa kushughulikia Mawasilisho kuhusiana na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na hivyo kuimarisha utekelezaji wa Tume wa mamlaka yake ya kulinda haki za binadamu. Mamlaka hayo yanaimarishwa zaidi na jitihada za Tume katika masuala ya dharura na ya muhimu ya haki za binadamu kupitia barua za kuomba majibu ya haraka, taarifa kwa vyombo vya habari, maazimio na barua za pongezi.

3. Mikutano ya kisheria na shughuli nyingine zilizorejelewa katika ripoti hii pia zilichangia katika kuongeza uhamasishaji wa haki za binadamu katika bara, kama inavyotakiwa na Mkataba wa Afrika, ikiwa ni pamoja na kupitia ziara za tume maalumu, ufafanuzi wa taratibu za nyongeza za haki za binadamu na nyaraka za maelezo, shughuli za ushawishi, utangazaji na kujenga uwezo.

4. Shughuli zinazofanywa na Vikundi Maalumu vya Tume na kujadili Ripoti za Nchi Wanachama wa Mkataba wa Afrika kuhusu utekelezaji wa haki na uhuru ulioainishwa katika Mkataba wa Afrika, zimechangia katika uboreshaji wa mifumo ya taifa ya kisheria na kitaasisi kwa ajili ya kuhimiza na kulinda haki katika ngazi ya taifa kupitia upitishaji wa sheria mpya, marekebisho ya sheria zilizopo na kuundwa au kurekebishwa kwa taasisi husika katika Nchi Wanachama. Pia, ripoti hiyo inawasilisha masuala yanayohusiana na fedha za Tume, watumishi waliopo na utendaji kazi wa Tume, pamoja na mapendekezo ya Tume kuhusu hali ya haki za binadamu katika bara.

Read More

More Documents

Working Document
REPUBLIC OF KENYA RESPONSE TO 58TH AND 59TH ACTIVITY REPORTS OF ACHPR_ENG.pdf
May 15, 2016
  • [EN ,PDF 1.68 MB]
Working Document
REPUBLIC OF ZIMBABWE RESPONSE TO 58TH AND 59TH ACTIVITY REPORTS OF ACHPR_ENG.pdf
May 15, 2016
  • [EN ,PDF 536.15 KB]
Working Document
EX CL 1659 (XLVIII)_Spa.pdf
May 15, 2016
  • [EN ,PDF 599.06 KB]
Working Document
EX.CL Dec.1327(XLVIII)ENG.pdf
May 15, 2016
  • [EN ,PDF 273.33 KB]
Working Document
EX CL Dec 1323 - 1351 (XLVIII)_FR.pdf
May 15, 2016
  • [FR ,PDF 271.06 KB]
Working Document
EX CL Dec 1327(XLVIII)PR.pdf
May 15, 2016
  • [PT ,PDF 200.40 KB]
Working Document
EX CL Dec 1327(XLVIII)AR.pdf
May 15, 2016
  • [AR ,PDF 209.55 KB]