Ripoti ya 54 na ya 55 ya Shughuli

No : 54-55
Type :
Activity Reports
Language :
Kiswahili
Publisher :
ACHPR

I.MUHTASARI

1.Ripoti ya 54 na ya 55 zilizounganishwa za Shughuli za Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu  (Tume au ACHPR) zinawasilishwa kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (UA), kwa mujibu wa Ibara ya 54 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu (Mkataba wa Afrika) na zinahusisha kipindi cha kuanzia tarehe 10 Novemba 2022 hadi tarehe 10 Novemba 2023 

2.Shughuli zilizowasilishwa katika Ripoti hii ambazo Tume ilifanya katika kipindi cha mapitio zimelenga kufikia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Tume wa 2021-2025. Kwa hiyo, mikutano ya kisheria ya Tume ililenga hasa kuimarisha mamlaka ya ulinzi kwa kushughulikia Mawasilisho kuhusiana na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na hivyo kuimarisha utekelezaji wa Tume wa mamlaka yake ya kulinda haki za binadamu. Mamlaka haya yanaimarishwa zaidi na uingiliaji kati wa Tume katika masuala ya dharura na ya muhimu ya haki za binadamu kupitia barua za kuomba majibu ya haraka, taarifa kwa vyombo vya habari, maazimio na barua za pongezi.

3.Pia inajumuisha shughuli zinazohusiana na uendelezaji bora wa haki za binadamu katika bara, kama inavyotakiwa na Mkataba wa Afrika.

4.Shughuli zinazofanywa na Vikundi Maalumu vya Tume na kujadili Ripoti za Nchi Wanachama wa Mkataba wa Afrika kuhusu utekelezaji wa haki na uhuru ulioainishwa katika Mkataba wa Afrika zimechangia katika uboreshaji wa mifumo ya sheria ya kitaifa   na kitaasisi kwa ajili ya uhimizaji na ulinzi wa haki katika ngazi ya kitaifa kupitia upitishaji wa sheria mpya, marekebisho ya sheria zilizopo na kuundwa au marekebisho ya taasisi husika katika Nchi Wanachama. Pia, ripoti hiyo inawasilisha masuala yanayohusiana na fedha, watumishi waliopo na utendaji kazi wa Tume, pamoja na mapendekezo ya Tume kuhusiana na hali ya haki za binadamu katika bara.

Read More