1. Banjul, Tarehe 27 mwezi wa Nane Mwaka 2023 - Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) imefanikiwa kuandaa na kufanya warsha ya kibara kwa siku mbili, iliyolenga hali ya watu wa jamii za asili barani Afrika, kutoka 25 hadi 26 Agosti 2023. Warsha hiyo iliitishwa na kuongozwa na Mheshimiwa Kamishna Dkt Litha Musymi-Ogana, Mwenyekiti wa Kikundi Kazi kinachohusika na Watu wa Jamii za Asili na Wachache Barani Afrika (WGIPM).
2. Warsha hiyo ilihudhuriwa na washiriki wasiopungua 115 ikiwa ni Pamoja na baadhi ya wajumbe wa Tume ya Africa, wawakilishi wa Nchi wanachama wa Umoja wa Africa, viongozi wa jadi, wawakilishi wa jamii za asili, watafiti, mashirika ya kiraia, Azaki, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa, pamoja na maafisa kutoka sekretarieti ya Tume..
3. Malengo Mhahususi ya warsha yalijikita katika utambuzi wa watu wa ya jamii za kiasili barani na kuainisha ujuzi wa kidaji katika mfumo wao wa ikolojia kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na maarifa ya asili, mazoea ya kitamaduni na jadi, sanaa na muziki, mifumo ya uzalishaji, uongozi wa jadi, ustamivi katika mazingira na maisha. Warsha hiyo ililenga kufungua uwezo wao, kuwawezesha na kuunda fursa za maendeleo kwao.
4. Warsha imefanikiwa kutambua vipaumbele muhimu vya afya itolewayo kwa mbali kwa jamii za asili, utambuzi wa vikundi vya jamii ya asili /idadi ya watu na uwasilishaji wake kwenye warsha ya uthibitisho utakaofanyika mnamo Mwezi Novemba 2023. Matokeo ya warsha yatawasilishwa baadaye.
5.Imetolewa na:
Secretariat, African Commission on Human and Peoples' Rights
31 Bijilo Annex, Western Region of North Kambo District.
P.O. Box 673
Banjul, Gambia
Tel.: 220 4410505/6
Fax: 4410504 220
Email: au-banjul@africa-union.org