TAARIFA KWA UMMA WARSHA LA KI BARA JUU YA HALI YA WATU WA ASILI KATIKA AFRIKA KUTOKA AGOSTI 25 HADI 26, 2023

share

Banjul, Gambia, 10 Agosti 2023 - Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu inaandaa warsha ya siku mbili, Warsha la ki Bara juu ya Hali ya Watu na Jumuhiya ya wa Asili barani Afrika, chini ya mamlaka ya Kikundi Kazi kinachohusika na Watu/Jumuihiya za watu wa Asili barani Afrika (WGIPM). Warsha hii inafanyika kwa mualiko wa Mheshimiwa Dkt. Litha Musimi-Oganna, Mwenyekiti wa Kikundi Kazi, kutoka 25 hadi 26 Agosti 2023

WGIPM inaandaa warsha hii kwa malengo mahususi, kufanya utambuzi wa jamii za asili barani Afrika na pia kutambua aina za maarifa wanayotumia kulinda mazingira yao kwa ujumla na hasa maarifa yao ya asili na ya kitamaduni, jadi, sanaa, muziki, mifumo ya uzalishaji na uongozi. 

Warsha hii imejikita katika kuwaleta pamoja wawakilishi wa serikali kutoka Afrika nzima na jumuiya na mashirika kikanda, taasisi za haki za binadamu, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanazuoni, na wadau wengine.

Unakaribishwa kujisajili kushiriki katika warsha hii kupitia kiungo kifuatacho: https://zoom.us/meeting/register/tJEpd-itqTkoHtRAOVNw06AR4B5woMigj7ZJ 

Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na:
Secretariat, African Commission on Human and Peoples’ Rights
31 Bijilo Annex Layout, Kombo North District Western Region.
PO Box 673
Banjul, The Gambia
Tel: 220 4410505/6
Fax: 220 4410504
E-mail: au-banjul@africa-union.org